::::


Kiongozi wa LRA nchini Uganda atiwa mbaroni.


Polisi nchini Uganda walimtia mbaroni Cesar Akalum mmoja wa viongozi wa jeshi la LRA( Lords Resistance Army) linalopigana na serikali ya Uganda , na kuongozwa na Joseph Kony ambae anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai. Vikosi vya Uganda (Uganda defence force) vimesema kuwa General Akalum ambae ni mmoja wa wakuu wa jeshi la Mola lililo na wafuasi kama 200, alikamatwa siku ya Jumamosi iliyopita nchini Afrika ya Kati. Inasemekana kuwa General Akalum alikamatwa akiwa pamoja na mkewe na binti yake.


 

 

 
 

 
Histori Kwa Kifupi :: Habari :: Michezo :: Sanaa :: Utalii :: maswala ya kimataifa :: wasiliana na sisi