Mpenzi msomaji: Assalam alaykum warahmatullahi wabarakatuhu.
Anaweza kuuliza muulizaji , kwa kuwa mnazungumzia miangaza juu ya elimu ya Qur an tukufu na kitabu kitukufu, basi nakuombeni mnijulishe ni zipi bora za kuhifadhia Qur an? Kwani mimi nina hifadhi na kusahau.
Mpenzi msomaji kabla sijakuelezea njia bora za kuhifadhi Qur an tuufu, napenda kuipitia njia ambayo walikuwa wakiitumia Maswahaba wa Mtume (s.a.w) katika kuhifadhi Qur an tukufu. Katika hadithi iliyopokelewa na Ibnu Ms-oud (R.A) amesema:
كنا إذا تعلمنا من النبي صلى الله عليه وسلم عشر آيات من القرآن الكريم لم نتعلم من العشر الذى نزلت بعدها حتى نعلم مافيه" أى حتى نعمل بما فى القرآن الكريم ونطبق أحكامه...
Ibnu Mas- oud anaseama , tulipokuwa tukijifundisha aya 10 kutoka kwa Mtume (s.a.w), basi tulikuwa hatujifunzi aya 10 zilizoshuka baadae ispokuwa mpaka tuzifahamu zile za kwanza, na kufahamu kuliko kusudiwa hawa hapa ni kuifanyia kazi Qur an na kutekeleza hukumu zake.
Mpaka hapa mpenzi msomaji tumefahamu njia bora za kuhifadhi Qur an ambazo ni, kwanza kuelewa maana yake, kasha kufanyia kazi yaliyomo ndani ya Qur an kwa kutekeleza hukumu zake.
Imam Ahmad ameelezea katika kitabu cha Zuhudi:
أن رجلا أتى أبا الدرداء فقال: إن ابنى جمع القرآن( يقصد أن ابنه حفظ القرآن) فقال أبو الدرداء : إنما جمع القرآن ( أى حفظ القرآن) من سمع له وأطاع.
Kuwa mtu mmoja alikwenda kwa Abou Al Dardaai akamwambia: hakika mwanangu amekusanya Qur an (akikusudia kuwa mwanawe amehifadhi Qur an) Abou Al Dardaai akamwambia kwamba, hakika alieikusanya Qur an( hifadhi Qur an) na alieisikiliza na kuitii.
Mpenzi msomaji hakika kufuata njia ya watu wema katika kuifahamu Qur an kwanza, kisha kuifanyia kazi, inasaidia sana katika kuhifadhi Qur an.
Pia katika njia zinazosaidia kuhifadhi Qur an ni mtu kuiheshimu Qur an, na kuwa Qur an hiyo siku ya qiyama iatamuombea mwenyekuisoma. Mtume ( s.a.w) anasema:
اقرؤوا القرآن فإنه يأتى يوم القيامة شفيعا لأصحابه
Someni Qur an kwani Qur an hiyo itakuwa muombezi kwa msomaji siku ya qiyama.
Ndugu msomaji hakika mwenye kuhifadhi Qur an atakuwa kwenye daraja ya juu peponi, na ataambiwa , soma na upande kama ulivyokuwa ukisoma duniani. Hakika miongoni mwa mambo yanayosaidia kuhifadhi Qur an kama wasemavyo wasomaji, ni kusoma kile ulichokihifadhi katika swala za sunnah , swala za usiku, kusoma mara kwa mara pale upatapo nafasi, na kusikiliza kanda.
Na wakati wa kuhifadhi Qur an kuna mambo unatakiwa kuyatambua vyema, nayo ni: nia safi, kujiepusha na maasi, maazimio ya kweli na kujitakasa kwa kuomba msaada wa M/Mungu. Na inakubidi kufuatilia kwa ukaribu kuhifadhi kwako na kurejelea yale uliyoyahifadhi kwa sheikh.
Na ili hifadhi yako iwe sahihi lazima usome sahihi, ikiwa ni pamoja na kudhibiti herufi vizuri, bila kusahau kurejelea ulichohifadhi kwani hawezi kuhifadhi bila kurejelea kile ulichokwisha kihifadhi. Na tambua kuwa wakati mzuri kwa kuhifadhi ni usiku na baada ya swala ya alfajiri.
Elewa pia kuna mambo yanaweza kumfanya mtu asihifadhi Qur an, na miongoni mwa mambo hayo ni wingi wa madhambi, kujishughulisha na mambo ya kidunia muda wote, kutofatilia na kutorejelea kile ulichohifadhi.
Mpenzi msomaji baada ya hayo kumbuka kuwa mwenye kuhifadhi Qur an anadaraja ya juu kwa M/Mungu, na Qur an hiyo itamuombea siku ya qiyama na mwenye kuhifadhi ni katika watu wa M/Mungu. Mambo yote haya yatakufanya uwe na nia thabiti wakati wa kuhifadhi kitabu cha M/Mungu.
اللهم اجعلنا من أهل القرآن, الحافظين, التالين لكتابك العزيز, وارفع درجاتنا يوم القيامة.
اللهم آمين . آمين