::::


SAFARI KATIKA ENEO LA SAKARA - ENEO LENYE HISTORIA YA KUVUTIA

Ktk eneo la Sakara ni eneo lililojawa na athari za kihistoia za kifirauni ambazo zipo na nyengine zinazoendelea kugunduliwa. Na gunduzi nyingi za ambazo zimejiri hivi karibuni.

Waziri wa nchi wa mambo ya kihistoria Dct. Zahy Hawaas amefungua makaburi 6 ya viongozi wakuu na mawaziri walioishi ktk enzi za baada ya zama za ujinga ktk eneo la Sakara, baada ya kumalizika kwa matengenezo maalum kwa ajili ya kutembelea sehemu hiyo. Na ktk hatua za matengenezo hayo kumegunduliwa nakshi za mbao ambazo zinarudi historia yake ktk ukoo wa 26. wakati ambapo matengenezo ya mara ya kwanza yalifanyika ktk miaka 500 kabla ya mizazi ya Yesu.

Moja ya makaburi hayo mpenzi msikilizaji ni kaburi la MUHIBU waziri ambae alimazikia kuwa mfalme wa mwisho wa ukoo wa 18. na pia kuna kaburi la MAYA ambae ni waziri wa hazina ya mfalme TUT-ONJ-AMOUN. Vile2 lipo kaburi la MIRI-NIIT. Huyu ni mhudumu wa jumba la ibada la AATON ktk enzi za mfalme ADHNATOUN. Pia lipo kaburi la BABI aliyekuwa mtumishi na muangalizi wa malkia wa mfalme TUT-ONJ-AMOUN. Na lipo kaburi la BATAAH- EM-WAYA ambae ni mmoja ktk wakuu wa baraza la kifalme ktk enzi za mfalme wa ukoo wa 18. na pia kaburi jengine ni la TIYAWATIYA ambae ni mfanyakazi ktk enzi za mfalme RAMSIS wa pili.


Na ktk mambo ya hubba ktk enzi za firauni, bwana MARINA BASIL Ana KAYOFONSKA wa nchini Brazil wametengeneza kisa cha kimapenzi kitakachokuwa miongoni mwa ngano za ulimwengu. Wawili hawa wamekubaliana kutangaza mpango huo ktk maeneo ya KATANA, utakaohusu MISRI NI UTAMADUNI MBELE YA ABUUL HUUL. Utakaotengenezwa ktk mandhari ya AHRAMAATI ya GIZA. Mpango huo umeshafikishwa kwa M/Kiti wa mambo ya Sinema, Mhandisi Iswaam Abdulhady na yuko tayari kuuhakikisha mpango huo ili kumshuhudia ABUL HUUL. Na ametoa muongozo mzima kuhusu mambo ya sauti, picha, machapisho pamoja na vazi maalum la kifirauni na ameamuru mpango huo uwe ktk mandhari ya maeneo ya AHRAMATI.


Kuyahakikisha maandiko adimu na ya kuvutia ktk usanifu wa kiislam
Dct Abdalla el Husein, waziri wa mambo ya wakfu ametangaza kuwa kamati shirikishi ya wizara mbili ya mambo ya wakfu na mawasiliano imemaliza utekelezaji wake wa protokoli ya ushirikiano kati ya wizara mbili hizo ktk kuuhakikisha urithi wa mambo ya wakfu ambao unajumuisha kuyathibitisha maandiko adimu na ya kuvutia ya usanifu wa kiislam. Waziri huyo amefafanua kuwa mpango huu una malengo ya kuyahifadhi mavutio ya kiislam kihistoria, kwa kuzingatia kuwa ni ukumbusho wa umma na unabeba jina la utamaduni wake. Jambo ambalo litawasaidia watafiti wanaopendelea kuchunguza mambo ya kale na historia yake. Na kwamba wizara ya mambo ya wakfu inamiliki hazina nyingi pamoja na maandiko ya kiislaam yaliyoadimu ambayo inapasa yahifadhiwe kwa mtindo wa kitaalam ili iwape faida watafiti mbali2 pamoja na wanafunzi.


 

 

 
 

 
Histori Kwa Kifupi :: Habari :: Michezo :: Sanaa :: Utalii :: maswala ya kimataifa :: wasiliana na sisi