::::


Karibu wakimbizi elfu moja wa Konbo ya kidemokrasia hukimbilia nchi jirani ya Rwanda kila kukicha.

Jamhuru ya Kongo ya Kidemorasia.
Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi imetangaza kuwa maelfu ya wakimbizi wa Kongo ya Kidemokrasia wamelazimika kuyakimbia makazi yao yaliyopo mashariki mwa Kongo ya Kidemokrasia kutokana na kuendelea kwa mapigano kati ya Jeshi la Kongo na makundi yenye kubeba mtutu wa bunduki karibu na maeneo hayo. Taarifa ya Kamisheni hiyo ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa karibu wananchi wa Kongo elfu ishirini waliyakimbia maeneo ya migogoro Mashariki mwa nchi hiyo na kuelekea katika mji wa Goma, ukiongezea na wengine zaidi ya elfu moja hukimbia na kuelekea nchi jirani ya Rwanda kila siku wakiikimbia hali ya usalama inayozorota pamoa na hali ya kiutu ndani ya nchi hiyo.


 

 

 
 

 
Histori Kwa Kifupi :: Habari :: Michezo :: Sanaa :: Utalii :: maswala ya kimataifa :: wasiliana na sisi