::::


Bi Banda asema Omar Albashiir hakaribishwi Malawi kwa kutakiwa kwake na mahakama ya jinai ya kitaifa.

Raisi wa Malawi Bi Joice Banda amesema kuwa raisi wa Sudani Omari Hasan Albashir anaetakiwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai kwa tuhuma za makosa ya kivita hakaribishwi kwenye mkutano wa kilele wa Afrika unaotazamiwa kufanyika mwezi wa Julai ujao na unaandaliwa nchini mwake. Akilizungumzia jambo hili, Bi Banda alisema kuwa anautaka Umoja wa Afrika kutoialika Sudani kuhudhuria mkutano huo wa Umoja waAfrika ambapo kiongozi huyo akarejea kusema kuwa nchi yake inakataa kumualika raisi wa Sudani Albashir kwa kuchelea vikwazo vya kiuchumi ambavyo huwenda nchi yake ikawekewa kutokana na hatua hiyo.


 

 

 
 

 
Histori Kwa Kifupi :: Habari :: Michezo :: Sanaa :: Utalii :: maswala ya kimataifa :: wasiliana na sisi