Viongozi wa kidini wawatolea wito wananchi kuyajali masilahi ya Taifa kuliko ya vyama yaliyofinyu.
Maimamu na Mashekhe wa chuo kikuu cha kiislamu cha Azhari pamoja na Wizara ya Mambo ya Dini wamesisitizia juu ya umuhimu wa kuyaweka masilahi ya nchi juu kuliko masilahi ya vyama na kusitisha haraka iwezekanavyo umwagaji damu na kutoitumia njia yoyote miongoni mwa njia za ubabe. Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Chuo Kikuu cha Azhari kimezitaka pande zote kuyatanguliza masilahi ya nchi mbele ya masilahi yoyote ya vyama yaliyofinyu. Jana yalizuka mapambano makali kati ya waandamanaji na majeshi ya kuweka usalama katika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi wakati wa majaribio ya baadhi ya waandamanaji kutaka kuvuka vizuizi vya usalama vilivyowekwa kuelielekea eneo linaloizunguka wizara hiyo na kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa.