Taifa la Mali lanukia kipindi chengine kipya cha mageuzi
Baraza la usalama la umoja wa nchi za Kiafrika (AU) limeyakaribisha maendeleo ya kushajihisha kurudisha utawala wa kiraia nchini Mali. Baraza hilo limeelezea kuridhishwa kwake baada ya raisi wa mpito bwana Dinkonda Traoure kupokea madaraka mwezi uliopita. Baraza hilo pia limetoa wito kwa pande zote nchini Mali kufuata utekelezaji wa vipengele vyengine vinavyojumuisha makubaliano ya dharura na ambayho yametiwa saini na pande zinazohusika. Baraza limesisitiza kuwa limeafikiana kufanya mkutano hivi karibuni ya kutoa maamuzi ambayo yanahitajika katika kuboresha hali ya mambo nchini Mali kulingana na utekelezaji wa makubaliano ya dharura yaliotiwa saini tarehe 6 Aprili mwaka huu.